Posted by: APO | 29 November 2012

Merck Inatoa Kidonge cha Milioni 100 Kutibu Skistosomasisi


Merck Inatoa Kidonge cha Milioni 100 Kutibu Skistosomasisi

Matibabu ya Skistosomasisi kwa watu wengi yaanza nchini Kenya

NAIROBI, Kenya, November 29, 2012/African Press Organization (APO)/ Merck (http://www.merckgroup.com), kampuni ya madawa, kemikali na sayansi ya uhai ya Ujerumani, leo imetoa kwa ishara kidonge cha milioni 100 praziquantel kwa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) katika uwezo wake wa ratiba ya ufadhili. Katika mkutano na waandishi wa habari Nairobi, Kenya, wawakilishi wa WHO na pia wa Merck walitangaza kuanzishwa kwa ugavi wa dawa hiyo kote nchini Kenya. Kenya ni nchi ya tano kote ulimwenguni ambamo ugonjwa wa Skistosomasisi umeenea zaidi. Kulingana na taarifa za WHO, zaidi ya Wakenya milioni 11, wengi wao wakiwa watoto, wanahitaji matibabu mwafaka/yafaayo.

Logo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/logos/merck_logo.jpg

Photo 1: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=333
(From left to right: Dr. Mark Bor, Permanent Secretary of the Kenyan Ministry of Public Health and Sanitation Dr. Rex Mpazanje, Acting Officer in Charge, WHO Kenya Dr. Stefan Oschmann, Merck Executive Board member and CEO Merck Serono)

Photo 2: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=334
(From left to right: Dr. Mark Bor, Permanent Secretary of the Kenyan Ministry of Public Health and Sanitation Dr. Rex Mpazanje, Acting Officer in Charge, WHO Kenya Dr. Stefan Oschmann, Merck Executive Board member and CEO Merck Serono)

“Kidonge cha milioni 100 kinaonyesha tukio muhimu katika ratiba yetu ya ufadhili tukishirikiana na WHO,” alisema Stefan Oschmann, mwanachama ya Bodi Tendaji wa Merck na Mkurugenzi Mkuu CEO wa Merck Serono. “Tangu Merck ilipoanza kufadhili WHO katika vita dhidi ya ugonjwa huu wa nchi za joto miaka mitano iliyopita, zaidi ya watoto milioni 28 wametibiwa katika nchi 11 za Afrika. Hata hivyo bado tuko mwanzo wa safari ndefu ambayo haitafika mwisho mpaka ugonjwa huu unaodhuru kisiri uangamizwe.” Mpaka sasa, Merck imekuwa ikilipa shirika la WHO hadi vidonge milioni 25 bila malipo kwa mwaka ambazo zina kirutubishi tendaji cha praziquantel. “Katika muda wa kadri, Merck itaongeza takwimu hiyo mara kumi hadi milioni 250 kwa mwaka. Kenya pia itafaidika kutoka kwa jambo hili,” Aliongeza Oschmann.

Katibu wa Kudumu wa wizara ya Afya ya Umma na Udhibiti wa Afya Bw. Mark Bor alikaribisha hatua hiyo ya kampuni ya Ujerumani: “Kujitoa kwa Merck hakutasaidia watoto walioathiriwa tu, bali pia itautia nguvu mfumo wetu wa utunzaji wa afya ya umma. Hii ni kwa sababu wagonjwa wasiotibiwa mara nyingi hupata matokeo mabaya ya kiafya ambayo husababisha mateso mengi yasiyokuwa ya lazima na kusababisha gharama kubwa.”

Custodia Mandlhate, akiwakilisha Mkurugenzi wa WHO inchini Kenya alisema, “Shirika la Afya Ulimwenguni limejiwekea shabaha ya kudhibiti na kuangamiza magonjwa ya maeneo ya joto yaliyopuuzwa, mmoja wapo ukiwa Skistosomasisi, kufikia 2020 ili lipate kuboresha na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote. Kwa hivyo, tunakaribisha kila hatua ya kudumu inayounga mkono jitihada zetu katika kupigana na magonjwa ya maeneo ya joto.”

WHO na Merck wataanza rasmi na ugavi wa praziquantel inchini Kenya kesho asubuhi katika shule iliyoko kilomita 80 kaskazini mashariki mwa Nairobi. Merck na wafanyikazi wa WHO watahusika katika sherehe ambapo maafisaa wa afya wa Kenya watatoa matibabu ya Skistosomasisi kwa watoto wa shule ya msingi ya Mouku kule Kirinyaga. Kulingana na kimo chao, watoto hupokea kati ya kidonge kimoja na vidonge vitano vya praziquantel. Ili tupate kupigana na ugonjwa huu vilivyo, matibabu lazima yarudiwe mara nyingi katika vipindi vya mwaka mmoja.

Skistosomasisi ni ugonjwa wa pili wa maeneo ya joto ulioenea zaidi barani Afrika baada ya malaria. Inakisiwa kwamba zaidi ya watu milioni 200 wameathiriwa na kwamba takribani 200,000 hufa kwa ugonjwa huo kila mwaka barani Afrika. Ugonjwa wa kuselelea, na kimelea husambazwa na minyoo (flatworms). Umeenea sana katika maeneo ya joto na maeneo yaliyo karibu nayo ambako watu maskini hawawezi kufikia maji masafi na vifaa vya kudhibiti usafi. Watu hushikwa na ugonjwa huu na mabuu ya minyoo sana sana katika maji baridi, kwa mfano wakifanya kazi, wakiogelea, wakivua samaki au wakifua nguo zao. Buu hilo dogo hupenya katika ngozi ya mwanadamu, na kukomaa kwenye ini na kuingia mishipa ya damu. Mayai yanayotagwa minyoo ya kike iliyokomaa hushikwa katika mkusanyiko wa seli na katika viungo vya ndani ambamo huchochea mijibizo ya kinga mwilini inayosababisha uharibifu na ugonjwa.

Praziquantel ndicho kirutubishi tendaji pekee ambacho kwacho kila aina ya Skistosomasisi inaweza kutibiwa. Kwa kuwa pia praziquantel huvumiliwa vizuri, pia iko katika orodha ya madawa muhimu ya WHO. Vidonge vyenye jina la Cesol® 600 kwa wakati huu yanatolewa katika kituo cha Merck nchini Mekisko.

Ratiba ya Merck ya Ufadhili wa Praziquantel ilizinduliwa 2007 ikishirikiana na WHO. Merck hutoa vidonge hivyo kwa WHO na hulipa gharama za usafirishaji hadi Afrika. WHO huendesha, hufuatilia na kunakili ugavi wa vidonge hivyo. Ongezeko kubwa katika idadi ya vidonge kutoka milioni 25 kwa mwaka wakati huu hadi milioni 250 katika muda wa kati litawezesha matibabu ya kama watoto milioni 100 kwa mwaka. Kujitolea kwa kifedha kwa ajili ya upanuzi wa Ratiba ya Merck ya Ufadhili wa Praziquantel itafikia kama USD milioni 23 kwa mwaka (takribani KES bilioni 1.9). Zaidi ya hayo, Merck pia inafadhili ratiba ya uhamasishaji katika shule zinazopatika sehemu mbali mbali Afrika kueleza sababu za Skistosomasisi kwa watoto na kuwafundisha jinsi ya kuzuia ugonjwa huo. Kwa sasa Merck inaendesha utafiti juu ya kupata fomula ya praziquantel ya watoto ambao hawajaenda shule katika mipaka ya ushirikiano kati ya umma na kampuni ya kibinafsi.

Distributed by the African Press Organization on behalf of Merck KGaA.

Gangolf Schrimpf

Phone +49 6151 72-9591

Taarifa zaidi juu ya vita dhidi ya Skistosomasisi zinapatikana katika kurasa za Merck na Shrika la Afya Ulimwenguni:

http://www.merckgroup.com/praziquantel

http://www.who.int/Schistosomiasis/en/index.html

Matoleo yote ya Habari ya Merck hugaviwa kwa kupitia kwa baruapepe na wakati huo huo hupatikana katika Tuvuti ya Merck. Tafadhali nenda http://www.merckgroup.com/subscribe ili ujisajili kwenye mtandao, badilisha chaguo lako au ukatishe huduma hii.

Merck (http://www.merckgroup.com) ni kampuni ya ulimwengu wote ya madawa na kemikali ikiwa ina jumla ya pesa bilioni € 10.3 mwaka wa 2011, historia iliyoanza 1668, na siku za usoni zinazochongwa na takribani wafanyikazi 40,000 katika nchi 67. Ufanisi wake imekuwa na sifa za uvumbuzi kutoka kwa wafanyikazi hodari.. Shughuli za Merck za kazi ziko chini ya Merck KGaA, ambamo jamaa ya Merck ina kama 70% ya riba na wenye shea wana milki zilizobaki ambazo ni kama 30%. Mwaka wa 1917 kitengo cha U.S. cha Merck & Co. kilitengwa na kimekuwa kampuni kivyake tangu wakati huo.

SOURCE

Merck KGaA


Categories