Posted by: APO | 22 October 2014

Shirika la ndege la flydubai linasherehekea ukuaji wake wa haraka katika Afrika Mashariki na uzinduzi wa safari mbili za ndege za Tanzania


Shirika la ndege la flydubai linasherehekea ukuaji wake wa haraka katika Afrika Mashariki na uzinduzi wa safari mbili za ndege za Tanzania

Njia hizo mpya zinasisitiza ukuaji wa haraka wa flydubai barani Afrika

DAR ES SALAAM, Tanzania, October 22, 2014/African Press Organization (APO)/ Uzinduzi wa safari za ndege za Dar es Salaam na Unguja za shirika la ndege la flydubai (http://www.flydubai.com) lililo na makao yake Dubai ziliwasili nchini Tanzania leo. Njia hizo mpya zinasisitiza ukuaji wa haraka wa flydubai barani Afrika, na kukuza mtandao wa shirika hilo la ndege mara mbili likiwa na vituo 12 mwaka huu.

Logo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/logos/flydubai.jpg

Photos: http://goo.gl/x4XwdY

flydubai iliingia soko hili mnamo 2009 na safari za ndege za Jibuti, na mnamo 2011 Addis Ababa ikawa kituo cha pili cha flydubai katika Afrika Mashariki. Mnamo 2014, flydubai iliongeza njia sita mpya barani humu kwa kuanzisha safari za ndege za kuenda Burundi, Rwanda, Uganda na vituo vitatu nchini Tanzania.

Akizungumza kuhusu uanzishaji wa safari za Tanzania, Ghaith Al Ghaith, Afisa Mkuu MTendaji wa flydubai, alisema: “Umoja wa Falme za Kiarabu umetambua uwezo mkubwa katika masoko yanayokua ya Afrika Mashariki, kama vile Tanzania. Tunaendelea kufanya kwa bidii kusaidia malengo ya usafiri, biashara na utalii kwa kuimarisha muungano wa moja kwa moja katika ya Umoja wa Falme za Kiarabu na masoko haya ya Afrika.”

Wawalikishi wa flydubai wakiongozwa na Sudhir Sreedharan, Naibu Mkuu wa Rais wa Biashra (GCC, Bara Dogo na Afrika), walilakiwa na tamasha za uzinduzi zilizofanyika katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam na Unguja mnamo 22 Oktoba 2014. Kati ya maofisa wakuu  waliozilaki ndege hizo za uzinduzi walikuwa Mheshimiwa Janet Z. Mbene (Mbunge), Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Dkt Omary Mjenga, Balozi Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu, Waziri wa Nchi.

“Kasi ya upanuzi wa safari za flydubai katika Afrika Mashaiki imeongezwa. Njia sita kati ya 23 mpya tulizozindua mwaka huu ziko barani Afrika. Uwezo tunaoona katika soko hili upeo mdogo wa uwezekano mkubwa kwani bado ni eneo ambalo halihudumiwi ipasavyo. Tuna furaha kuhusu safari zetu mpya za ndege nchini Tanzania, zitakazokuwa maarufu sana na abiria wetu ikiwa ni wa starehe au biashara,” alisema Sreedharan.

Hivi karibuni Tanzania imeibuka kama mbia muhimu wa kibiashara wa Dubai na ni kati ya wabia wakubwa wa biashara zisizo za mafuta barani Afrika ikifikisha Dola bilioni 1.86 za Marekani mwaka jana katika jumla ya mapato ya biashara ya mwaka, hii ni kulingana na bata mypa kutoka Chama cha Wafanyabiashara cha Dubai.

flydubai ilianza kutumia ndege zake mpya za Boeing 737-800 zilizo na Kitengo cha Biashara katika safari zake za Dar es Salaam, Kilimanjaro na Unguja kuanzia tarehe 16 Oktoba, 2014, ikiwapa abiria kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu huduma rahisi sana, ya kiwango cha juu na ya kuaminika iliyo na chaguo ya kuunganisha safari kuelekea kitovu cha safari za anga Dubai.

Zaidi ya safari zake tatu nchini Tanzania, flydubai imeunda mtandao mpana barani Afrika na safari za ndege za Addis Ababa nchini Uhabeshi, Alexandria nchini Misri, Khartoum na Port Sudan nchini Sudani, mji mkuu wa Jibuti, Juba nchini Sudani Kusini pamoja na Bujumbura nchini Burundi, Entebbe nchini Uganda na Kigali nchini Rwanda.

Maelezo ya Safari za Ndege:

Dar es Salaam

flydubai itakuwa na safari za ndege za kila siku kati ya Dar es Salaam na Dubai kuanzia tarehe 16 Oktoba 2014.

FZ670 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 6:20 machana saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:55 jioni saa za ndani.

FZ672/674 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 12:20 jioni saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani.

FZ669/671/673 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 5:20 asubuhi saa za ndani.

Nauli za safari ya pande mbili

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Dar es Salaam hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1,499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli spesheli za uzinduzi zitakazotumika kwa mwezi mmoja.

Kilimanjaro kupitia Dar Es Salaam

flydubai itakuwa na safari mbili za ndege kwa wiki kati ya Kilimanjaro na Dubai kupitia Dar Es Salaam kuanzia tarehe 17 Oktoba 2014.

Jumatatu na Ijumaa:

FZ674 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro saa 10:10 jioni saa za ndani, itue Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

FZ673 imepangwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro saa 7:25 saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

Nauli za safari ya pande mbili

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Kilimanjaro hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1,499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli spesheli za uzinduzi zitakazotumika kwa mwezi mmoja.

Unguja kupitia Dar es Salaam

flydubai itakuwa na safari mbili kwa wiki kati ya Unguja na Dubai kupitia Dar es Salaam kuanzia tarehe 19 Oktoba 2014.

Jumanne na Ijumaa: FZ672 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Unguja saa 9:40 mchana saa za ndani, itue Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

FZ671 imepangwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Unguja saa 7:05 mchana saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

Nauli za safari ya pande mbili

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Unguja hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1,499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli spesheli za uzinduzi zitakazotumika kwa mwezi mmoja.

Tiketi zinaweza kununuliwa kuanzia leo kutoka kwa tovuti ya flydubai (flydubai.com), Kituo chake cha Ndani cha Simu +255 (22) 2124005, maduka ya usafiri ya flydubai au kupitia wabia wa usafiri. Taarifa na maelezo zaidi ya huduma za shirika hili za ukodishaji gari na bima ya safiri pia zinaweza kupatikana kwenye flydubai.com.

Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of flydubai.

Media contact:

mediarelations@flydubai.com

Kuhusu flydubai:

Shirika la ndege lenye makao yake Dubai linajikakamua kuondoa vizuizi vya usafiri na kuimarisha uhusiano kati ya tamaduni tofauti katika mtandao wake unao endelea kukua. Tangu uzinduzi wa biashara yake mnamo 2009, flydubai (http://www.flydubai.com):

•          Imeunda mtandao wa vituo 86, pamoja na safari 20 mpya zilitangazwa 2014.

•          Imefungua safari 54 mpya ambazo hapo awali hazikuwa na safari za moja kwa moja hadi Dubai au hazikuwa zinahudumiwa na shirika la kitaifa la Umoja wa Falme za Kiarabu kutoka Dubai.

•          Imeunda msafara wa ndege 41 mpya za Boeing 737-800 New Generation na inasubiri kuwasilishwa kwa zaidi ya ndege 100 ifikapo mwisho wa 2023.

Zaidi ya hayo, wepesi na urahisi wa flydubai kama shirika changa la ndege umeimarisha ukuaji wa uchumi wa Dubai, kufuatana na dira ya Serikali ya Dubai, kwa kuanzisha mtiririko wa biashara na utalii katika masoko ambayo hayakuwa na huduma hizi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma za flydubai, tafadhali tembelea http://www.flydubai.com.

Charting the Dynamic Rise of flydubai: http://www.apo-mail.org/141022.PDF

Fact Sheet: http://www.apo-mail.org/1410222.PDF

flydubai at a glance: http://www.apo-mail.org/1410223.PDF

flydubai Route Map: http://www.apo-mail.org/1410224.pdf

flydubai Cargo Route Map: http://www.apo-mail.org/1410225.pdf

SOURCE

flydubai


Categories

%d bloggers like this: