Posted by: APO | 12 September 2014

Madagaska imeongezwa kwenye mtandao unaokua wa Air Seychelles


Madagaska imeongezwa kwenye mtandao unaokua wa Air Seychelles

VICTORIA, Seychelles, September 12, 2014/African Press Organization (APO)/ Air Seychelles (http://www.airseychelles.com), shirika la ndege la kitaifa la Jamhuri ya Ushelisheli, imetangaza leo uzinduzi wa safari za moja kwa moja hadi Antananarivo, Madagaska, kuanzia tarehe 3 Desemba 2014.*

Logo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/logos/as.png

Sagari hizi  mbili kwa wiki hadi Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa capital’s Ivato (TNR) zitakuwa zikiendeshwa kwa kutumia ndege ya Airbus A320 yenye vitengo viwili na viti 16 vya kitengo cha Biashara na 120 vya kitengo cha Uchumi.

Madagaska inajulikana kwa vivutio vyake vya kipekee vya mimea na wanyama, hasa Maeneo tatu ya Urithi Duniani ya UNESCO —msitu wa mvua wa Atsinanana, Hifadhi Asili ya Tsingy de Bemaraha , na Mlima wa Kifalme wa Ambohimanga, kituo cha kiroho cha watu wa Merina.

Huduma hizi mpya zitaifanya hii kuwa nchi ya nne ya Air Seychelles katika mtandao wa kimkoa unaokua haraka ambao unajumuisha Dar es Salaam, Johannesburg na Mauritius.

Manoj Papa, Afisa Mkuu Mtendaji wa Air Seychelles, alisema:  “Tunafuraha sana kuongeza Antananarivo kwenye mtandao wetu mkuu, kwa njia hiyo tunaimarisha  msimamo wetu kama shirika linalopendelewa katika mkoa wa Bahari Hindi.

“Madagaska inafurahisha ukuaji dhabiti wa uchumu kutokana na uwekezaji wa kigeni na utalii wa mazingira.  Ndege zetu zitashughulikia hitaji linalokua la usafiri wa biashara na burudani kwa kisiwa ambacho ni cha nne kikubwa zaidi duniani.

“Njia hii itaboresha biashara na utalii katika njia zote, na hasa, inakaribishwa na idadi kubwa ya watu wa Malagasi wanaoishi Ushelisheli, ambao sasa wana njia rahisi ya kuwatembelea marafiki na familia nyumba ni.

“Kupitia kitovu chetu cha Mahé, tutawapa wageni  wanaotoka Madagaska njia nyingine nzuri za visiwa vingi vya Ushelisheli, kwa kuongezea maeneo yanayohuduiwa na ndege zetu katika Mashariki ya Kati, Ulaya na Asia, na hata pia na washirika wetu wa ‘codeshare’.”

Ndege ya A320 itatoa pia tani saba za mizigo ya kusafirisha kila wiki kwenda na kutoka Madagaska, ambayo ina soko dhabiti la mizigo inayoingia na kutoka.  Shirika hili linatarajia kubeba mchanganyiko wa vitu vinavyoweza kuharibika au kuoza, vipuri vya kiufundi na dawa katika njia hii.

Joël Morgan, Waziri wa Ushelisheli wa Mambo ya Nyumbani na Uchukuzi na Mwenyekiti  wa Bodi ya Air Seychelles, alisema safari hizi mpya ni kiashirio cha mafanikio ya Air Seychelles, na hata pia umuhimu wa Ushelisheli kama kitovu kipya cha eneo.

“Bahari Hindi ni kitovu cha maendeleo ya mtandao wetu wa njia, na tunafuraha kuwa sasa Antananarivo ni sehemu ya mtandao wa Air Seychelles.  Inaashiria hatua muhimu katika mkakati wetu wa kupanuka katika eneo hili.

“Mapema mwaka huu, Ushelisheli na Madagaska ilitia saini Makubaliano mapya ya Huduma za ndege, ambapo matoleo yaliyoboreshwa yamewezesha moja kwa moja utangazaji wa safari hizi.

“Safari ya moja kwa moja hadi Antananarivo itafungua nafasi mpya kwa serikali, biashara, utalii na mabadilishano ya kitamaduni katika Bahari Hindi, na kupitia mtandao wetu mkuu, tutaunganisha eneo hili kwa dunia.

“Tunatoa pia chaguo za ratiba mpya kwa wasafiri, kwa hivyo kutoa chaguo na urahisi zaidi katika eneo hili, na kufanya hazina ya kupendeza ya utamaduni,  mkusanyiko wa wanyama, na mimea kufikiwa zaidi kwa walio kwenye likizo, iwe ni wanaokuja hapa tu au wanaochanganya na ziara nyingine kwa visiwa vingine vya eneo, kama vile Comores, Mayotte, Mauritius, or Réunion.”

Huduma ya Air Seychelles kuelekea Antananarivo, inastahili kuanza tarehe 3Desemba 2014: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/photos/tablesw.png

*inategemea vibali vya serikali

Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of Air Seychelles.

Maswali ya Vyombo vya Habari

Alan Renaud, Meneja Mkuu wa Masuala ya Kampuni

Simu: +248 2525741

Barua Pepe: arenaud@airseychelles.com

Kuhusu Air Seychelles

Air Seychelles (http://www.airseychelles.com) ilianzishwa mwaka wa 1978 na ilianza huduma yake ya safari ndefu mwaka wa 1983. Shirika hili linatoa sasa safari za kimataifa hadi Abu Dhabi, Hong Kong, Johannesburg, Mauritius and Paris. Air Seychelles hutoa pia safari zaidi ya 200 zilizoratibiwa za kindani kwa wiki katika archipelago na hata pia huduma za kukodisha za kindani.  Kama shirika la ndege la kitaifa la Jamhuri ya ushelisheli, Air Seychelles ni nguzo ya utalii, sekta dhabiti na inayokua ya kiuchumi ya taifa hili la kisiwa. Shirika hili la ndege linadumisha ushirikiano wa kimkakati na Etihad Airways, shirika kuu la ndege la taifa la Muungano wa Falme za Kiarabu na lenye asilimia 40 la hisa. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.airseychelles.com.

SOURCE

Air Seychelles


Categories

%d bloggers like this: