Posted by: APO | 28 September 2012

Viongozi wa afrika washirikiana na viongozi wa dunia kusukuma ukuaji wa kilimo katika Afrika


Viongozi wa afrika washirikiana na viongozi wa dunia kusukuma ukuaji wa kilimo katika Afrika

Mkutano wa Mageuzi ya Kilimo cha Afrika waanza mjini Arusha Tanzania

ARUSHA, Tanzania, September 28, 2012/African Press Organization (APO)/ Viongozi wa mataifa ya Afrika, mawaziri,wawakilishi wa sekta za kibinafsi, jamii ya kimataifa, na wakulima, walikongamana hivi leo kwenye mkutano wa Shirika la Mageuzi ya Kilimo cha Afrika – African Green Revolution Forum (AGRF) (http://www.agrforum.com) mjini Arusha, Tanzania, kubainisha mikakati thabiti ya utekelezaji juu ya mbinu za kugeuza sekta ya kilimo cha Afrika. AGRF 2012 ni jukwaa la dunia kwa ajili ya kutangaza sekta hii ya uwekezaji wa kibinafsi na maongozi ya ufadhili kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za kilimo na ukuaji wa mapato kwa sekta ya kilimo cha Afrika.

Event Photo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/photos/agrf-opening.jpg (Melinda Gates, Rais Jakaya Kikwete wa Tananzia na Kofi Annan kwenye mkutano wa Mageuzi ya Kilimo cha Afrika mjini Arusha Tanzania)

Logo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/logos/agrf.jpg

Akiwa mwenyeji wa mkutano huu, MH. Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aligusia juu ya matumaini mema ya Afrika katika siku zijazo kwa wajumbe wa Mkutano huo.

“Tuna mwelekeo wa kuweza kupata ufanisi katika juhudi zetu za kuangamiza njaa na umaskini katika Afrika, kupitia njia ya mageuzi ya kilimo.”alisema Rais Kikwete. “Kwa mchanganyiko wa maongozi bora, kuchukuliwa kwa maamuzi sawa na serikali za mataifa yetu ya Afrika, uendelevu wa misaada kutoka kwa wafadhili na kushiriki kikamilifu kwa sekta ya kibinafsi katika nchi zetu na kwingineko kadhalika, mageuzi ya kilimo cha Afrika yanaweza kufikiwa.”

Akifungua mkutano huo, Kofi Annan, Mwenyekiti wa Umoja wa Mageuzi ya Kilimo cha Afrika – Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) alieleza juu ya ufanisi uliofikiwa tangu mkutano wa kwanza wa AGRF mnamo mwaka wa 2010. Bw. Annan pia alisisitiza juu ya umuhimu wa kuwaboresha wakulima wa mashamba madogo kwa kuwasaidia kwenda mbele kupelekea mazingira ya kilimo cha biashara.

“Lengo letu la kuongeza uzalishaji na faida kwa wakulima wa mashamba madogo – wengi wao wakiwa ni wanawake – haliwezi kuyumba. Wao ndio wanaotuwekea chakula kwenye meza zetu, Wao ndio wanaotunza rasilamali zetu za ardhi na maji” alisema Bw. Annan. Hatimaye, wao ndio watakao sukuma ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Afrika katika karne ya 21.”

Melinda Gates, Mwenyekiti mshiriki wa Wakfu wa Bill & Melinda Gates, ambaye alikwenda Arusha kuhutubia wajumbe wa mkutano huu, alitambua maendeleo makubwa ya kilimo cha Afrika yaliyofikiwa ndani ya muda wa muongo mmoja uliopita, na akatoa wito kwa viongozi wa Afrika waendelee kuunga mkono juhudi hizo.

“Nawahimiza viongozi wa Afrika kuzingatia upya ahadi zenu za kuongeza uzalishaji wa jamii ya wakulima. Nawahimiza kuweka ajenda ya muongo ujao, itakayokuwa na ari kubwa zaidi,” alisema Bi. Gates. “Natumai mtakuwa makini kweli kuhakikisha kwamba ahadi na mipango yenu itapelekea kuwasaidia jamii za wakulima hawa kufikia malengo yao.”

Distributed by the African Press Organization on behalf of the African Green Revolution Forum (AGRF).

Contact – Deanna Petersen, +27 29 702 8033 or dpetersen@webershandwick.com

Juu ya AGRF (@agrforum; #AGRF2012)

Shirika la Mageuzi ya Kilimo cha Afrika – African Green Revolution Forum (AGRF) (http://www.agrforum.com) limelenga kuimarisha uwekezaji na maongozi ya ufadhili kwa kusukuma uzalishaji wa kilimo na ukuaji wa mapato ya wakulima wa Afrika katika mazingira ya njia ya uendelevu. Shirika hili ni chimbuko la maongozi ya sekta ya kibinafsi linalojumuisha washikadau mbali-mbalikujadiliana na kuimarisha mipango kabambe ya uwekezaji kwa ajili ya kufikia mageuzi ya kilimo cha Afrika. Washiriki wa misimamo thabiti ni pamoja na AGRA(http://www.agra-alliance.org), Yara International (http://www.yara.com), Umoja wa Afrika (http://www.au.int) na Shirika lake la Mipango na Ushirikishi NEPAD (http://www.nepad.org).

SOURCE

African Green Revolution Forum (AGRF)


Categories

%d bloggers like this: